Isaiah 4


1 aKatika siku ile wanawake saba
watamshika mwanaume mmoja
wakisema, “Tutakula chakula chetu wenyewe
na kuvaa nguo zetu wenyewe,
ila wewe uturuhusu tu tuitwe kwa jina lako.
Utuondolee aibu yetu!”

Tawi La Bwana

2 bKatika siku ile Tawi la Bwana litakuwa zuri na lenye utukufu, nalo tunda la nchi litakuwa fahari na utukufu wa wale Waisraeli watakaonusurika. 3 cWale watakaoachwa Sayuni, watakaobaki Yerusalemu, wataitwa watakatifu, wale wote ambao wameorodheshwa miongoni mwa walio hai huko Yerusalemu. 4 dBwana atausafisha uchafu wa wanawake wa Sayuni, atatakasa madoa ya damu kutoka Yerusalemu kwa Roho ya hukumu na Roho ya moto. 5 eKisha Bwana ataumba juu ya Mlima wote wa Sayuni, na juu ya wale wote wanaokusanyika hapo, wingu la moshi wakati wa mchana, na kung’aa kwa miali ya moto wakati wa usiku, nako juu ya huo utukufu wote kutatanda kifuniko cha ulinzi. 6 fUtakuwa sitara na kivuli kutokana na joto la mchana, na kuwa mahali pa kujificha kutokana na dhoruba na mvua.
Copyright information for SwhKC